SHULE YA SEKONDARI NA UFUNDI LUA

MKUU WA SHULE YA SEKONDARI NA UFUNDI LUA

Iliyopo Ulongoni ’A’ Gongolamboto jijini Dsm, anapenda kuwatangazia wazazi, walezi na vijana waliohitimu shule ya msingi, kuwa shule ya Lua ina nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2024 kwa elimu ya sekondari ya kawaida na ufundi kwa pamoja. Shule ya LUA ni kati ya shule chache nchini zilizokidhi vigezo vya serikali vya kutoa elimu ya sekondari ya kawaida na elimu ya AMALI au UFUNDI STADI kwa wakati mmoja kwa kutumia mtaala ulioboreshwa na serikali unaofuata sera ya elimu ya mwaka 2014 toleo la 2023. Mzazi/mlezi/kijana mhitimu wa elimu ya msingi, zinduka sasa! jiunge na sekondari itakayokupa elimu mbili kwa mpigo! Yaani elimu ya sekondari na elimu ya ujuzi. Waaombaji wa nafasi katika shule hii watakuwa na nafasi ya kuchagua kusomea elimu ya sekondari ya kawaida na moja ya fani za ufundi stadi zifuatazo; 1. UMEME yaani Electrical Installations na 2. UFUNDI MAGARI yaani Motor Vehicle Mechanics. Baada ya kuhitimu kidado cha nne, wahitimu watatunukiwa cheti cha elimu ya sekondari kutoka NECTA na cheti cha ufundi kutoka NACTVET. Huu ni wakati wa kujibu kilio cha wazazi cha muda mrefu cha kumpeleka mtoto shuleni kwa miaka minne halafu anarudi nyumbani pasipo na ujuzi wowote.

Pia tunawakaribisha vijana waliomaliza kidato cha nne kujiunga na kozi katika fani za umeme na ufundi magari pamoja na udereva. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0768 62 1111 au 0715 015 778. LUA SECONDARY

Related Posts

Comments